Marekani na Ulaya Zaiwekea Rwanda na AFC/M23 Shinikizo Kusitisha Mapigano Mashariki ya Congo
Marekani na nchi kadhaa za Ulaya zimezitaka Rwanda na AFC/M23 kusitisha mara moja operesheni za kijeshi Mashariki mwa Congo, zikionya kuwa mapigano yanayoendelea Kivu Kusini yanaweza kuhatarisha usalama wa eneo lote. Mataifa haya yamesisitiza umuhimu wa kurejea kwenye makubaliano ya amani ya Doha na kuondolewa kwa vikosi vya RDF kwenye ardhi ya Congo.
Marekani pamoja na baadhi ya nchi za Ulaya zimeongeza shinikizo kubwa dhidi ya kikundi cha AFC/M23 na Jeshi la Rwanda (RDF) wanalishinja kukiunga mkono, zikazitaka pande zote mbili “kusitisha mara moja” mashambulizi yanayoendelea katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Mbali na Washington, nchi nyingine zimo katika kundi rinalishinikiza Rwanda na AFC/M23, zikiwamo Umoja wa Ulaya (EU), Ujerumani, Ubelgiji, Uingereza, Ufaransa, Uholanzi, Denmark, Uswisi na Sweden.
Haya yaje wakati mapigano mapya yakongezeka wiki iliyopita katika Jimbo la Kivu Kusini, baina ya AFC/M23 na muungano wa majeshi ya Serikali ya DR Congo, ukiwemo FARDC, Jeshi la Burundi, FDLR na wanamgambo wa Wazalendo.
Vikosi vya M23 vinavyoongozwa na Jenerali Sultani Makenga, baada ya zaidi ya wiki moja ya mapigano makali, viliweza kuteka maeneo kadhaa muhimu, ikiwamo Jiji la Uvira jiji la pili kwa ukubwa katika Kivu Kusini ambako waliingia Jumanne jioni, tarehe 9 Desemba.
Mapigano yanaendelea kushika kasi Mashariki mwa Congo, wakati ambapo Alhamisi iliyopita Rais Félix Antoine Tshisekedi alisaini makubaliano ya amani na mwenzake Paul Kagame wa Rwanda.
Katika taarifa ya dharura iliyotolewa kwa pamoja, Marekani na nchi za Ulaya zilisema zina "wasiwasi mkubwa kuhusu machafuko yanayoendelea karibu na mpaka wa Burundi," zikionya kuwa yanaweza kuhatarisha utulivu wa eneo lote.
Mataifa hayo yalizitaka AFC/M23 na RDF kusitisha mashambulizi dhidi ya majeshi yanayopambana na kikundi hicho, yakisema: “Tunazitaka AFC/M23 na Jeshi la Rwanda (RDF) kusitisha mara moja operesheni zao za kijeshi Mashariki mwa Congo, hususan katika Kivu Kusini, na pia tunaitaka RDF kuondoka kwenye ardhi ya Congo.”
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilisisitiza pia kuwa AFC/M23 inapaswa “kurudi katika maeneo yake ya awali na kuunga mkono makubaliano ya msingi” ambayo ilisaini pamoja na Serikali ya Kinshasa mjini Doha, Qatar.
Nchi hizo pia zilionyesha wasiwasi kuhusu matumizi ya “ndege zisizo na rubani za kujitoa muhanga (suicide drones)”, zikibainisha kuwa matumizi yake yanaashiria kuongezeka kwa kiwango hatari cha mashambulizi na kuweka raia katika hatari kubwa.


Kinyarwanda
English
Swahili



