Tetesi za Soka Ulaya: Messi Kusaini Mkataba Mpya Inter Miami, Chelsea Yamnyatia Omorodion, Bruno Fernandes Kuvunja Ukimya

Oct 20, 2025 - 12:22
 0

Habari za hivi punde kutoka soka la Ulaya: Lionel Messi anatarajiwa kusaini mkataba mpya na Inter Miami, Chelsea yajiandaa kutoa zaidi ya €100m kwa Samuel Omorodion, huku Bruno Fernandes akifikiria kuondoka Manchester United mwishoni mwa msimu. Soma tetesi zote za usajili, mipango ya vilabu vikubwa na habari za wachezaji barani Ulaya leo kupitia UkweliTimes.

Mshambuliaji nyota wa Argentina Lionel Messi, mwenye umri wa miaka 38, anatarajiwa kusaini mkataba mpya na klabu ya Marekani Inter Miami, kwa mujibu wa taarifa za mwandishi wa habari mashuhuri Fabrizio Romano.

Klabu za Arsenal na Tottenham Hotspur zinaripotiwa kuwa miongoni mwa vilabu vya Ligi Kuu ya England vinavyomfukuzia mshambuliaji chipukizi wa Saint-Etienne, Djylian N’Guessan, mwenye umri wa miaka 17. (Caught Offside)

Luis Milla, kiungo wa kati wa Kihispania mwenye umri wa miaka 31 anayechezea Getafe, amevutia macho ya kocha wa Aston Villa Unai Emery pamoja na meneja wa Atletico Madrid Diego Simeone msimu huu. (Fichajes – kwa Kihispania)

Klabu ya Chelsea inadaiwa kuwa tayari kutoa zaidi ya euro milioni 100 (£87m) ili kumsajili mshambuliaji wa Uhispania, Samuel Omorodion, mwenye umri wa 21, kutoka klabu ya Porto katika dirisha lijalo la usajili. (Fichajes – kwa Kihispania)

Wachezaji wa zamani wa Manchester United — Eric Cantona, Wayne Rooney na David Beckham — wameombwa kuwasilisha ombi la kuinunua klabu hiyo kupitia muungano wa wawekezaji kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE). (The Guardian)

Wapelelezi wa vipaji wa Barcelona walikuwa wakimfuatilia Mason Greenwood, mshambuliaji wa zamani wa England mwenye umri wa 21, baada ya kufunga mabao manne akiwa na Marseille mwishoni mwa wiki. (TBR Football)

Meneja wa Fulham, Marco Silva, anatajwa kuwa chaguo la kwanza la Nottingham Forest kuchukua nafasi ya Ange Postecoglou, lakini anaripotiwa kusita kuondoka Craven Cottage katikati ya msimu. (The Times – usajili unahitajika)

Klabu ya Bournemouth inajiandaa kupokea ofa kutoka kwa vilabu vinavyotaka kumsajili mshambuliaji wa Ghana Antoine Semenyo, mwenye umri wa 25, katika dirisha lijalo la usajili. (Football Insider)

Vilabu vya Newcastle United na Aston Villa vinapigiwa upatu kumsajili mlinzi wa Ecuador Joel Ordonez, mwenye umri wa 21, kutoka klabu ya Club Brugge. (Caught Offside)

Casemiro, kiungo wa kati wa Brazil mwenye umri wa 33, anatarajiwa kupewa mkataba mpya na Manchester United, ingawa mkataba huo utahitaji kupunguzwa kwa mshahara wake mkubwa wa sasa. (Football Insider)

Nahodha wa Manchester United Bruno Fernandes anafikiria kuhama klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu endapo hawataonyesha maendeleo. Klabu ya Bayern Munich inatajwa kuwa na nia ya kumsajili kiungo huyo wa kati wa Ureno mwenye umri wa 31. (Fichajes – kwa Kihispania)

Layla kamanzi Layla Kamanzi is a passionate journalist and creative writer with a keen eye for impactful storytelling. As a Journalism and Mass Communication student at Mount Kenya University, she is dedicated to using words as a tool to inform, inspire, and amplify the voices of everyday people. Driven by curiosity and a love for truth, Layla explores stories that shape communities and spark meaningful conversations. She enjoys blending facts with compelling narratives to create content that educates, empowers, and connects audiences across East Africa and beyond.