AFC/M23 Yadhibiti Maeneo ya Uvira Kati ya Mapigano Mazito ya Kivu Kusini

Dec 9, 2025 - 12:59
 0

AFC/M23 imeripotiwa kuingia na kudhibiti maeneo muhimu ya Jiji la Uvira, ikiwemo Mulongwe na Kasenga, baada ya kusukuma nyuma vikosi vya FARDC, askari wa Burundi, Wazalendo na FDLR. Haya yamefuatia kutwaa Kiliba na Luningu, hatua iliyowafungulia njia kuelekea Uvira. Hadi sasa, hakuna tamko rasmi la serikali ya DRC kuhusu maendeleo haya, huku wakazi wakibaki katika wasiwasi na sintofahamu juu ya usalama wa eneo hilo.

Taarifa kutoka kwa vyanzo mbalimbali vya raia na wachunguzi wa masuala ya usalama katika Jimbo la Kivu Kusini zinathibitisha kuwa kikundi cha AFC/M23 tayari kimeingia na kudhibiti maeneo kadhaa ya Jiji la Uvira, mji ulioko karibu sana na mpaka wa Burundi, ukerekezwa kutoka Bujumbura.

Mashahidi wanaripoti kuwa vikosi vya FARDC, askari wa Burundi, wapiganaji wa Wazalendo pamoja na wanamgambo wa FDLR wamelazimishwa kurudi nyuma kutoka maeneo waliyokuwa wakiyashikilia, kufuatia mapigano makali ambayo yamekuwa yakiendelea kwa siku kadhaa. Taarifa zinaendelea kuonyesha kuwa AFC/M23 imekwisha kutwaa Mulongwe, Kasenga, pamoja na maeneo mengine ya jirani ndani ya mji wa Uvira.

Haya yanajiri baada ya mapema leo asubuhi AFC/M23 kutwaa eneo la Kiliba na Luningu, maeneo yanayotajwa kuwa muhimu katika barabara inayotoka Bonde la Rusizi kuelekea Uvira. Udhibiti wa maeneo haya umeufungulia umoja huo njia ya haraka kuelekea Jiji la Uvira, jambo lililoongeza wasiwasi juu ya hali ya usalama wa eneo hilo.

Hata hivyo, hadi sasa hakuna tamko lolote rasmi kutoka Serikaliy ya DRC wala uongozi wa kijeshi wa taifa kwenye ngazi ya kimataifa lililothibitisha au kukanusha taarifa hizi za mapigano. Taarifa zinaendelea kufuatiliwa na vyombo husika, huku wakazi wakibaki katika hali ya sintofahamu na hofu kuhusu usalama wao.

Layla kamanzi Layla Kamanzi is a passionate journalist and creative writer with a keen eye for impactful storytelling. As a Journalism and Mass Communication student at Mount Kenya University, she is dedicated to using words as a tool to inform, inspire, and amplify the voices of everyday people. Driven by curiosity and a love for truth, Layla explores stories that shape communities and spark meaningful conversations. She enjoys blending facts with compelling narratives to create content that educates, empowers, and connects audiences across East Africa and beyond.