Madagascar: Jeshi Latangaza Kuchukua Madaraka Baada ya Maandamano ya Vizazi vya Gen-Z

Oct 14, 2025 - 21:43
 0

Jeshi la CAPSAT nchini Madagascar limetangaza kuchukua madaraka baada ya maandamano makubwa yaliyoongozwa na vijana wa kizazi cha Gen Z kupinga utawala wa Rais Andry Rajoelina. Hatua hiyo inakuja baada ya bunge kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye. Kanali Michael Randrianirina amesema jeshi litaunda kamati ya mpito ya kijeshi na kiraia, huku likiahidi uchaguzi ndani ya miaka miwili ijayo. Rais Rajoelina hajatoa kauli, na ripoti zinaonyesha huenda amekimbia nchi.

Jeshi la CAPSAT nchini Madagascar, ambalo zamani lilimsaidia Andry Rajoelina kupanda madarakani, sasa limemgeuka, huku Kanali Michael Randrianirina akitangaza rasmi kwamba jeshi hilo limechukua mamlaka ya nchi.

Mnamo mwaka 2009, CAPSAT (Corps des Personnels et des Services Administratifs et Techniques) lilimuunga mkono Rajoelina alipompindua aliyekuwa rais wakati huo, Marc Ravalomanana. Sasa, hali imegeuka baada ya maandamano makubwa yaliyoanza tarehe 25 Julai 2025 yakipinga utawala wa Rajoelina, maandamano ambayo yameongozwa na vijana wa kizazi cha Gen Z.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, wanajeshi wa CAPSAT walijiunga na maelfu ya waandamanaji waliokuwa wakiipinga serikali ya Rajoelina, ishara wazi ya mgawanyiko mkubwa ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama.

Haya yametokea mara tu baada ya bunge la Madagascar kufanya kura ya kumng’oa rais madarakani. Hata wabunge kutoka chama cha Rajoelina, IRMAR, walishiriki katika kura hiyo na wengi wao wakapiga kura kumuondoa madarakani.

Baada ya tangazo la kuchukua madaraka, Kanali Randrianirina alisema kuwa CAPSAT itaunda kamati ya kijeshi itakayojumuisha maafisa wa jeshi, polisi, na kijeshi cha jandarma.

Aliongeza kuwa, “Huenda baadaye tukaongeza wajumbe wa kiraia katika kamati hii. Kamati hiyo ndiyo itakayotekeleza majukumu ya urais kwa muda.”

Aidha, alisema serikali ya mpito itakayoundwa hivi karibuni itakuwa na uwakilishi wa kiraia.

Kanali Randrianirina pia alisisitiza kuwa vijana wa kizazi cha Gen Z  waliokuwa mstari wa mbele katika maandamano  watashirikishwa katika mabadiliko haya kwa sababu, “Mapambano haya yalianzia mitaani, hivyo ni lazima tusikilize matakwa yao.”

Alifafanua kuwa wao kama jeshi hawakuwa na njia nyingine ila kuiondoa serikali iliyokuwa madarakani:

“Hakuna rais, hakuna serikali... kila kitu kimesimama nchini.”

Jeshi Latangaza Kuchukua Madaraka Baada ya Maandamano ya Vizazi vya Gen-Z

Alitangaza pia kuwa jeshi hilo limesitisha kwa muda taasisi zote zilizoundwa kwa mujibu wa katiba, isipokuwa bunge lililopiga kura ya kumuondoa rais.

Taasisi zilizofutwa kwa muda ni pamoja na seneti, mahakama ya katiba, na tume ya uchaguzi  kama ilivyoripoti shirika la habari la Reuters.

Jeshi hilo lilitangaza kuwa baada ya miaka miwili, taifa litafanya uchaguzi mkuu wa kidemokrasia.

Hadi sasa, Rais Andry Rajoelina hajatoa tamko lolote kuhusu hatua hii ya jeshi.

Habari zinaeleza kuwa huenda tayari amekimbia nchi, ingawa haijathibitishwa rasmi.

Kabla ya kura ya bunge ya kumwondoa madarakani, Rajoelina alikuwa amejaribu kulivunja bunge kupitia tangazo alilochapisha kwenye mtandao wa X, lakini juhudi hizo hazikufanikiwa.

Layla kamanzi Layla Kamanzi is a passionate journalist and creative writer with a keen eye for impactful storytelling. As a Journalism and Mass Communication student at Mount Kenya University, she is dedicated to using words as a tool to inform, inspire, and amplify the voices of everyday people. Driven by curiosity and a love for truth, Layla explores stories that shape communities and spark meaningful conversations. She enjoys blending facts with compelling narratives to create content that educates, empowers, and connects audiences across East Africa and beyond.