Vita vya Iran : Amerika imeongeza muda wa kusitisha mashambulizi dhidi ya Iran

Apr 22, 2026 - 01:34
 0

Rais wa Marekani, Donald Trump, ametangaza kuwa usitishaji wa mapigano utaendelea hadi pale mazungumzo ya kumaliza vita kati ya Marekani na Iran yatakapokamilika. Vita hivyo vimekaribia kufikisha miezi miwili tangu vianze.

‎Hatua hiyo imechukuliwa kufuatia ombi la Pakistan, nchi ambayo imekuwa ikiratibu mazungumzo kati ya Tehran na Washington. Wakati huo huo, Trump amesema kuwa ataendelea kuweka vikwazo, ikiwemo kufunga bandari za Iran.

‎Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye mitandao ya kijamii.

‎“Kutokana na hali dhaifu ya Iran, pamoja na ombi la Marshal Asim Munir na Waziri Mkuu wa Pakistan, Shehbaz Sharif, tumekubaliana kusitisha mashambulizi hadi viongozi wa Iran watakapowasilisha rasimu ya makubaliano ya pamoja.” Trump alisema

‎Aidha, alieleza kuwa ameagiza jeshi la Marekani kuendelea kuwa katika hali ya tahadhari huku likidhibiti bandari za Iran.

‎“Usitishaji mapigano utaendelea hadi rasimu ya makubaliano itakapowasilishwa na mazungumzo kufikia hitimisho, kwa njia moja au nyingine,” aliongeza.

‎Mapema alfajiri ya tarehe 8 Aprili 2026, Trump alikuwa tayari ametangaza makubaliano ya muda ya kusitisha mapigano kwa kipindi cha wiki mbili kati ya Marekani na Iran.

‎Hatua hiyo ilifuatia zaidi ya mwezi mmoja wa mapigano makali yaliyoanzishwa na Israel kwa kushirikiana na Marekani dhidi ya Iran. Vita hivyo vilisababisha vifo vya viongozi kadhaa wakuu wa Iran, akiwemo Ali Khamenei.

‎Mgogoro huo umeathiri kwa kiasi kikubwa uchumi wa dunia, hasa baada ya Iran kufunga njia ya Strait of Hormuz, inayopitisha takriban asilimia 20 ya mafuta ya dunia. Kufungwa kwa njia hiyo kumesababisha kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la kimataifa.

‎Bei ya pipa moja la mafuta ilipanda kutoka takriban dola 70 hadi kufikia dola 120 mwezi Machi 2026, kabla ya kushuka kidogo. Hivi karibuni, bei hiyo iliongezeka tena kwa asilimia 5 na kuvuka dola 100 kwa pipa. Baada ya tangazo la Trump kuhusu kuendelea kwa usitishaji mapigano, bei ilishuka hadi dola 98.97.

‎Mnamo tarehe 21 Aprili 2026, Trump alionya kuwa Iran inaweza kukumbwa na matatizo makubwa ambayo haijawahi kuyashuhudia iwapo haitakubali kuingia katika mazungumzo na Marekani.

‎Akizungumza katika mahojiano na mwandishi wa habari John Fredericks, Trump alisema kuwa vita hiyo iko karibu kumalizika, lakini akasisitiza kuwa mustakabali wake utategemea uamuzi wa Iran. Hata hivyo, Iran bado haijaonyesha wazi kama iko tayari kushiriki katika mazungumzo, ikieleza kuwa ina mashaka na msimamo wa Washington kuhusu demokrasia.

Manishimwe Janvier Political Journalist II Communication Specialist ll Tel:+250785584281

Vita vya Iran : Amerika imeongeza muda wa kusitisha mashambulizi dhidi ya Iran

Apr 22, 2026 - 01:34
Apr 22, 2026 - 10:09